Assalamu’alaikum
Amani tamu ya Mwenyezi Mungu na iwe nanyi leo. Iweni na maarifa ya Neno lake pamoja na Neno hilo kukaa ndani yenu.
.
Kuna swali moja ambalo Waislamu wote wenye mawazo mapana wanapaswa kujiuliza wakati kwa wakati. Ni dhahiri sana kutoka katika Kurani Tukufu and kutoka katika Vitabu Vitakatifu, kwamba Israeli wa Kale, yaani, Wayahudi, wakati fulani walikuwa watu wateule wa Mwenyezi Mungu. Kwa nini, basi, walikataliwa baadaye? Hivi ilikuwa ni kwa sababu walikataa kuziona ishara dhahiri za Mwenyezi Mungu kama zilivyooneshwa kwao katika Maandiko ya Agano la Kale?
Sura 5:44 “Hakika tuliteremsha (kwa Musa) Taurati yenye uongozi na nuru; ambayo kwayo Manabii waliojisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu) waliwahukumu Mayahudi: na watawa na maulamaa pia (walihukumu kwa hiyo Taurati), kwa sababu walitakiwa kuhifadhi Kitabu (hicho) cha Mwenyezi Mungu; nao walikuwa mashahidi juu yake. Basi (ninyi Waislamu) msiwaogope watu, bali niogopeni (mimi). Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache (ya duniani). Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.”
005.044 Al-Maidah
Walikosa nini Wayahudi? Kwa nini walikataliwa wasiwe watu wateule wa Mwenyezi Mungu? Je, hawakuwa watu wale ambao Mwenyezi Mungu alikuwa amefanya kazi pamoja nao kwa miaka zaidi ya elfu moja? Kwa majibu haya tutaangalia vile Vitabu vitakatifu ambavyo Mwenyezi Mungu aliviteremsha kuwa uongozi na mauidha kwetu. Lakini kwanza, kipaumbele chetu ni kumwomba msomaji kupeleka dua lake kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwa hatupaswi tu kumtii Yeye, bali pia kumtazamia atupe ufahamu. Tusipokuwa na Roho (Ruh) wake Mwenyezi Mungu kutuongoza sisi ni hakika tutaishia katika makosa. Sisi hatuna hekima yetu wenyewe, hivyo twahitaji kuangalia mbinguni ili kupata msaada. Msaada kama huo tutapewa kama kwa unyenyekevu tutatafuta hekima itokayo mbinguni.
Masihi Isa alitabiriwa…
Ni dhahiri kwamba Mwenyezi Mungu hakupenda Wayahudi wakataliwe, wala kwamba wao wamkatae Masihi Isa! Mwenyezi Mungu alitabiri kwa wazi katika Maandiko ya Kiebrania jinsi Masihi ambavyo angekuja. Twapenda kuziona baadhi ya Aya ambazo manabii wa kale waliwafunulia Wayahudi katika Maandiko ya Agano la Kale, na kisha jinsi zilivyotimizwa ili pasiwepo na haja ya mtu awaye yote kukosea kujua ni nani hasa aliyekuwa Masihi Isa!
Masihi Isa angekuwa nabii kama Musa. Hayo yaliandikwa karibu na mwaka wa 1451 K.K. Kumbukumbu zikiwa zimeandikwa katika Vitabu Vitakatifu vya Taurati. Katika Kumbukumbu la Torati 18:15 Musa aliandika… “BWANA, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye.”
Unabii huu ulitimizwa katika maisha ya Masihi Isa. Katika Injili Matendo 3:20-22 iliyoandikwa karibu na mwaka 33 B.K. inasema hivi kumhusu Isa… “(Mwenyezi Mungu) apate kumtuma Kristo Yesu, … Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi.”
Kwamba Masihi Isa angezaliwa na bikira ilitabiriwa pia kwa wazi na nabii Isaya. Karibu katika mwaka ule wa 742 K.K. Isaya 7:14 “Tazama, bikira atachukua mamba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.”
Unabii huu ulitimizwa karibu na mwaka 5 K.K. umeandikwa katika Injili unasema: Mathayo 1:18,21 “Mariamu … alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu [Ruh wa Mwenyezi Mungu].”
Hata mahali halisi kilipokuwapo kijiji alimokuwa azaliwe Masihi Isa kilitabiriwa waziwazi. Nabii Mika katika Taurati. Mika 5:2 katika mwaka wa 742 K.K. [alitabiri hivi:] “Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele…”
Katika kumbukumbu zilizo katika Injili twaona kutimia kabisa kwa unabii huu wa zamani… Mathayo 2:1 ukitokea katika mwaka wa 5 K.K. “Yesu (Isa) alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi.” Katika Israeli ile ya zamani palikuwa na vijiji viwili vilivyoitwa Bethlehemu, kwa hiyo kuwa na hakika kwamba kijiji sahihi kilitambulishwa nabii Mika alieleza wazi kuwa kingekuwa ni kile cha Bethlehemu ‘Efrata’.
Nabii Daudi pia alitabiri kwamba Wafalme kutoka Mashariki wangekuja kumwabudu Isa na kutoa zawadi zao kwake za thamani kubwa. Katika Zaburi 72:10 imeandikwa… “Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.” Twaona kwamba hayo yalitimia katika Mathayo 2:2,11 karibu na mwaka wa 4 K.K. “Mamajusi (Wenye Hekima) walitoka Mashariki kuja Yerusalemu kumwabudu, walimpa zawadi: dhahabu na uvumba na manemane.”
Kuhusu kazi yake ambayo Masihi Isa angeweza kuifanya ilitabiriwa pia waziwazi. Mwaka 713 K.K. Taurati, Isaya 35:5,6 “Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa. Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba…”
Unabii huu ulitimizwa katika mwaka ule wa 31 B.K. Injili Mathayo 11:4-6 “Yesu (Isa) akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana (Yahya) mnayoyasikia na kuyaona; vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema.”
Nabii Daudi hata aliandika katika Zaburi kwamba Isa angekataliwa na Wayahudi. Zaburi 118:22 “Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni.”
Yakiwa yametimizwa katika Injili Mathayo 21:42. “Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika Maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, nalo ni ajabu machoni petu.”
Ukweli kwamba yule aliyekuwa karibu sana miongoni mwa wanafunzi wake Isa angemsaliti mikononi mwa watu wasiomcha Mungu ulikuwa umetabiriwa wazi na Daudi katika Zaburi. Zaburi 41:9 “Msiri wangu tena niliyemtumaini, aliyekula chakula changu, ameniinulia kisigino chake.”
Hilo lilitimizwa: Injili Yohana 13:18-21. “Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu ameniinulia kisigino chake.…Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti [maneno haya yanamhusu Yuda Iskariote ambaye usiku ule ule alimsaliti Isa kwa makuhani wa Kiyahudi.]”
Nabii Isaya alitabiri kwamba maadui zake Isa wangemtendea jeuri. Yakiwa yameandikwa katika mwaka ule wa 712 K.K. Taurati Isaya 50:6 “Naliwatolewa wapigao mgongo wangu, na wang’oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate.”
Hayo yalitimia katika Injili: Injili Marko 14:65 “Wengine wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, na kumpiga makonde.” Yohana 19:1 “Basi ndipo Pilato alipomtwaa Yesu, akampiga mijeledi.” [Akaruhusu apigwe mijeledi]
Nabii wa kale Zekaria alitabiri kwamba Isa angepigwa, kisha wafuasi wake wangetawanyika. Mwaka 487 K.K.. Taurati Zekaria 13:7 “Mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika.”
Hilo lilitimizwa katika mwaka wa 33 B.K. [31 B.K. kwa Kalenda ya sasa] katika Injili imeandikwa: Mathayo 26:56 “Ndipo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.”
Nabii Zekaria hata alitabiri juu ya kiasi cha fedha ambacho Wayahudi wangemlipa Yuda kwa kumsaliti kwao. Taurati Zekaria 11:12 “Mkiona vema, nipeni ujira wangu; kama sivyo, msinipe. Basi wakanipimia vipande thelathini vya fedha, kuwa ndio ujira wangu.”
Hayo yalitimia katika mwaka 33 B.K. [31 B.K. kwa Kalenda ya sasa]. Injili Mathayo 26:15 “Wakampimia [Yuda] vipande thelathini vya fedha.” Pia Mathayo 27:3-5 “Kisha Yuda … akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia. … Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu…”
Kutokana na ushahidi wote huu na mengi zaidi ambayo tungeweza kusimulia, yaonekana kuwa ni jambo la ajabu kwamba Wayahudi wangemkataa Yeye ambaye aliteremshwa chini. Lakini yatupasa kutambua kuwa Isa hakuja kama Wayahudi walivyotarajia aje. Wao walitaka mtawala ambaye angewafukuzilia mbali Waroma kutoka katika nchi yao. Isa aliposhindwa kufanya vile walikataa kumtambua. Isa alitumwa akiwa na utume tofauti na ule. Alipaswa kuwa kafara (dhabihu) kwa ajili ya dhambi za wanadamu wote. Nabii Isaya alitabiri katika mwaka ule wa 712 K.K. kwamba Isa atazichukua dhambi za watu wote. Taurati Isaya 53:4-6 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu … Alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu. … Na BWANA ameweka juu yake maovu yetu sisi sote.”
Hayo yalitimia katika Injili Mathayo 20:28 “Mwana wa Adamu [alikuja] kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.”
Lakini Wayahudi wale wa zamani waliyakataa hayo yote, na hatimaye ulifika wakati ambapo Isa aliwaambia… “Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.” Injili Mathayo 23:38 Mwenyezi Mungu aliliacha Hekalu pamoja na Taifa lile. Katika mwaka wa 69 B.K. Tito, Mroma, akaja na kuuharibu Yerusalemu, na Hekalu lile tukufu and zaidi ya milioni moja ya Wayahudi. Fundisho hili la kihistoria ni kwa ajili yetu sisi.
Mpendwa mtumishi wake Mwenyezi Mungu, leo na tuipokee fidia yake kwa ajili ya dhambi zetu. Na tusiwe kama Wayahudi wale wa kale waliomkataa yule aliyeteremshwa. Lakini ni afadhali tupokee Toleo hili la Rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambaye ni Masihi Isa. Hebu kwa unyenyekevu tutii, na kupokea cho chote kinachoteremshwa kutuokoa sisi milele. Tunao mfano dhahiri wa Wayahudi mbele yetu ambao walikataa kile alichokiteremsha Mwenyezi Mungu. Isa alikuwa ndiye ushahidi wenye nguvu kabisa kuonesha kwamba Mwenyezi Mungu angeweza kumteremsha, naye alikataliwa. Hatuwezi kumudu kufanya yale yale pasipo kukabiliwa na hasara ile ile ya milele. Leo hii Mwenyezi Mungu na akupe wewe amani ya milele na milele zote.
Aya Zimenukuliwa kutoka DivineIslam’s Qur’an Viewer software v2.913
Maandiko ya Biblia yanatoka katika Toleo la King James (KJV)
Kwa maelezo zaidi: www.salahallah.com
Kwa Nini Mwenyezi Mungu aliwakataa Israeli wa Kale!
Mfululizo na. 25